Kuhusu HolyStore!
HolyStore ni mfumo wa kielektroniki wa uliobuniwa, kuhaririwa na kutengenezwa kwa lengo la kurahisisha uhifadhi na uchakataji wa taarifa na kumbukumbu mbalimbali za uratibu na uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kanisa katoliki, kuwaleta waumini karibu na kuwapa fursa na uhuru wa kuwasiliana na kujadili mambo mbalimbali ya kiroho miongoni mwao
Mfumo huu umetengenezwa kwa kufuata misingi halisi ya kanisa katoliki, bila kubadili au kuleta dosari yoyote katika mfumo na mwongozo uliopo wa kuratibu shughuli za kanisa
Mfumo unamfikia mtumiaji mkatoliki, kuanzia ngazi ya jumuiya hadi ngazi ya parokia ikijumuisha makundi mbalimbali ya kiroho ndani ya kanisa
Ukiwa umegawanyika katika sehemu kuu mbili, HolyStore - Parokia na HolyStore - Karismatiki, ikiwa lengo ni kutoa huduma bora kwa idara zote ndani ya taasisi ya kikatoliki
